Waandishi wa habari hapa nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari zenye kuondoa mitazamo potofu ndani ya jamii, ya kumuona mwanamke hawezi kuwa kiongozi.
Hayo yamezungumza leo Septemba 19, 2019 na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, wakati akifungua mafunzo ya Siku tatu kwa wandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, yanayoendeshwa na mtandao huo kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wanahabari hao, namna ya kuandika habari za kijinsia katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.
Amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa sana katika kutumia kalamu zao kuandika habari zenye kuiondoa jamii juu ya mitazamo hiyo Potofu ya kumtazama mwanamke kama kiumbe dhaifu, na hatimaye kumpatia nafasi ya kuwa kiongozi katika nyazifa mbalimbali.
“Lengo la mafunzo haya ni kujenga na kuongeza uelewa na uwezo wa waandishi wa habari, katika kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi,” amesema Liundi.
“Kuna baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikimkwamisha mwanamke katika kupewa nafasi za uongozi, ikiwamo mfumo dume, na mitazamo potofu ya kumwona mwanamke kama kiumbe dhaifu, hivyo ni wakati kwa waandishi wa habari kutumia Kalamu zenu ipasavyo, ili kubadilisha mitazamo hiyo ili kufikia 50 kwa 50 katika nafasi za uongozi,”ameongeza.
Aidha amesema kwa takwimu za mwaka 2018 hadi januari 2019 zinaonyesha wanawake wakuu wa nchi wapo 10 kati ya 152, wakuu wa Serikali wapo 10 kati ya 193, ambapo kwa Afrika nzima Ma-Rais wanawake wapo wawili tu, na kubainisha usawa wa kijinsia ukitekelezwa ipasavyo nchi itaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Naye mwezeshaji kwenye mafunzo hayo ya masuala ya kijinsia Beatrice Ezekiel, amewataka waandishi hao wa habari kulitokomeza kabisa tatizo la mfumo dume, ambalo limekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya jamii pamoja na kuandika habari za mfumo wa kijinsia kwa kuonyesha takwimu.
Aidha mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro, Mara, Geita, Rukwa, Pwani,Ruvuma, Tabora, pamoja na Shinyanga, ambayo yanafanyika kwenye Hotel ya Silver Paradise Jijini Dar es salaam.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini juu ya kuandika habari zenye kuhamasisha wanawake kushiriki nafasi za uongozi na kuondoa mitazamo potofu kwa jamii dhidi yao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mwezeshaji wa mafunzo ya masuala ya Kijinsia Beatrice Ezekiel akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari zenye mrengo wa kijinsia.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za kijinsia na kuhamasisha wanawake na vijana kushiriki kwenye nafasi za uongozi.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Mwandishi wa habari Israel Mwaisaka kutoka Nkasi FM -Rukwa akiwasilisha kazi ya kwenye kikundi chake.
Mwandishi wa habari Costansia Michael kutoka Top Radio Morogoro akiwasilisha kazi ya kwenye kikundi.
Mwandishi wa habari Michael Joackim kutoka Nkasi FM-Rukwa akiwasilisha kazi ya kwenye kikundi.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akipiga picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, kwenye mafunzo ya kuongeza uelewa na uwezo kwa wana habari kuripoti masuala ya kijinsia katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Social Plugin