Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Kimataifa Wa Sheria Kati Ya Afrika Na Asia | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 24, 2019

Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Kimataifa Wa Sheria Kati Ya Afrika Na Asia

  Malunde       Tuesday, September 24, 2019
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu kutoka nchi za Afrika na Asia ambao kwa pamoja wataangalia maendeleo ya sekta ya sharia na kujadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na jinsi ya kukabiliana nazo.

Prof.Mchome amesema katika mkutano huo Tanzania itakabidhiwa kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye atatumikia kiti hicho kwa mwaka mmoja.

Prof. Mchome alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Serikalini Ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijijini Dodoma ambao aliwaomba kuuungana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha Mkutano huo utakaoitangaza nchi kimataifa unafanikiwa.

AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika.

Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana  uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.

Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 na kwa sasa Katibu Mkuu wake ni Mtanzania Prof. Gastorn ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo mwezi Agosti 2016.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post