IGP Sirro Awacharukia Maofisa wa Jeshi la Polisi......"Acheni Ubinafsi, Mimi ndo IGP na Kama Unaona Sitoshi Subiri Zamu Yako Mungu Akipenda" | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 24, 2019

IGP Sirro Awacharukia Maofisa wa Jeshi la Polisi......"Acheni Ubinafsi, Mimi ndo IGP na Kama Unaona Sitoshi Subiri Zamu Yako Mungu Akipenda"

  Malunde       Tuesday, September 24, 2019
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewaeleza maofisa wa Jeshi hilo kuwa mara nyingi kinachowasumbua ni ubinafsi na kuwaambia haiwezekani wote wakawa ma-IGP "There is no way" kwani yeye hakujichagua.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 24, 2019 wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Mkuu na Makamanda wa mikoa.

Akizungumza na viongozi hao IGP Sirro amesema wakati mwingine wapo wanaona kama yeye hatoshi.


"Wakati nikiwa ninazungumza mwingine anaona hatoshi huyu, ninatosha mimi, kama unajiona kama unatosha na Mungu hakukupa sasa si ukubali sasa mimi nitafanyaje?, hakuna njia ya kunisema nikasema sasa atajuaje kama mimi sitoshi, kamanda wa Kinondoni (Mussa Taibu) unanipata vizuri umenisikia sasa naenda mwaka wa tatu bado unafikiria, kubali yaishe itafika mahali Mungu akiona unatosha atakupa," amesema.

Amesema wakati huu bado Mungu ameona hata kama uwezo wake ni mdogo lakini ndiyo amempa.


"Itafika wakati nami nitaondoka na ninamuomba Mungu nikiondoka niliache Jeshi la Polisi likiwa na heshima yake" Amesema

Katika hatua nyingine IGP Sirro amelipongeza jeshi lake kwa namna ambavyo limeweza kupambana na kukomesha mauaji ya raia yaliyokuwa yakifanyika Wilayani Kibiti mkoani Pwani.

''Habari ya Kibiti ndani ya Jeshi la polisi haitofutika, issue ilikuwa ni kubwa sana na kwa challenge jeshi la polisi,  lakini slogan yetu ya umoja ndiyo nguvu yetu ndio imetufikisha hapa tulipo. 


"Sasa hivi ukizungumzia Kibiti hata viwanja vimepanda bei, wanasiasa wanafanya siasa zao ni heshima ya jeshi lakini pia ni heshima kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama'', amesema


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post