TAMASHA LA 14 LA JINSIA KUFANYIKA SEPTEMBA 24 HADI 27 DAR


Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa nguvu za pamoja Anna sangai akitoa ufafanuzi wa jambo mapema jana jijini Dar es salaam katika semina za jinsia na maendeleo.

TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Wanasemina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wanakuletea Tamasha la 14 la Jinsia linalotarajiwa kufanyika septemba 24 mpaka 27 Makao makuu ya shirika hilo Mabibo jijini Dar es salaam.

Akizungumzia tamasha hilo Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja Anna Sangai amesema tamasha la mwaka huu litaenda sambamba na vitu viwili vikubwa navyo ni, miaka 25 TGNP Mtandao pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Mkutano wa Beijing.

Aidha amesema sababu ya kuunganisha matukio hayo kwa pamoja ni kutokana na kuwa kabla ya mkutano wa Beijing hapa nchini hapakuwa na jukwaa huru na rasmi la kukutana washiriki wa Tanzania, ndipo waliamua kuunda Mtandao wa Jinsia Tanzania ili kuweza kukutana na kujadili mambo yao kama wanaharakati wa haki za wanawake.

Ameongeza kuwa tamasha la mwaka huu ambalo litakuwa na washiriki zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo ameeleza washiriki watatoka katika nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Zambia Jamhuri ya watu wa Congo nk.

Pia tamasha la mwaka huu litakuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “Wanaharakati wa jinsia mbioni kuibadilisha dunia”

Amesisitiza kuwa lengo kuu la tamasha hilo litakalodumu kwa siku takribani 4 ni kukutana kwa pamoja na wadau wa masuala ya jinsia kuweza kujadili changamoto mbalimbali, kusherehekea mafanikio pamoja na kufanya tathmini au mchanganuo toka walipoanza na walipo kwa sasa, na hii ni pamoja na kuweka mikakati mingine mipya ili kufikia malengo wanayotarajia kuyafikia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527