POLISI MWANZA WAZUNGUMZIA TUKIO LA WACHIMBAJI KUFUKIWA NA KIFUSI

Ajali Ya Gema Machimboni  Kuporomoka Na Kusababisha Kifo Na Majeruhi.

Tarehe 9/9/2019 Majira Ya 01:00hrs Katika Machimbo Ya Dhahabu Shilalo,yaliyopo Kata Ya Inonelwa Wilaya Ya Misungwi Mkoa Wa Mwanza Wachimbaji Wadogo Wakiwa Kwenye Shughuli Zao Za Kawaida Za Uchimbaji Mdogo Wa Madini Ya Dhahabu Katika Duara Namba 50 Mali Ya Deogratius S/o Lushanga Na Duara Namba 47 G Mali Ya Peter S/o Charles, Duara Zilizo Kuwa Na Wachimbaji  Takribani Kumi Ambao Ni;

 Ndaki S/o Juma 45yrs, Msukuma, Nyamikoma-busega, Keo S/o Werema 34yrs, Mkurya, Mkazi Wa Mahanga B Bunda, John S/o Katwale, 35yrs, Mwasagera-misasi, Mwita S/o George 27yrs, Mkurya, Makazi Bunda, Masanja S/o Charles, 42yrs, Mkazi Wa Ishokela, Abdala S/o Abdu, 38yrs, Mkazi Wa Nyangomango Misungwi, Bengwe S/o Clenent, 29yrs, Msukuma, Mkazi Wa Kabale, Songa S/o Charles, 28yrs, Msukuma, Mkazi Wa Kabale, Emmanuel S/o Mathias, 34yrs, Msukuma, Mkazi Wa Salawe Shinyanga Na Mang’era S/o Meki, 40yrs, Mkazi Wa Mwanza.

Wakati Wakiendelea Na Uchimbaji Ndani Ya Maduara Hayo Ghafla Gema La Udongo Lilimeguka, Likaporomoka Na Kuanguka Kisha Kufunga Njia Za Maduara Hayo. 

Juhudi Za Haraka Zilifanyika Na Kufanikiwa Kuwaokoa Watu Wanane Wakiwa Hai,wakiwa Na Majeraha Mbalimbali  Na Mtu Mmoja Alikutwa Amefariki Ambae Ni Ndaki S/o Juma Na Jitihada Za Kumuokoa Mtu Aitwaye Keo S/o Werema Zinaendelea Kufanyika. 

Majeruhi Walifikishwa Hospitali Ya Wilaya Misungwi Kwa Matibabu Na Maiti Imehifadhiwa Hospitalini Kwa Hatu Za Uchunguzi.

Tukio La Pili;  Tarehe 06/08/2019 Majira Ya 07:00hrs Huko Mtaa Wa Kagera Jirani Na Shule Ya Msingi Kagera Wilaya Ya Ukerewe  Kulitokea Tukio La Mauaji Ambapo Euzebia D/o Didakus@ Malas 16yrs, Mwanafunzi Kidato Cha Tatu Shule Ya Sekondari Nansio Aliuawa Kwa Kukatwa Na Kitu Chenye Ncha Kali Kichwani. Jeshi La Polisi Limefanikiwa Kumkamata Joseph S/o Msafiri @anthon, Msukuma 30yrs Mkazi Wa Mtaa Wa Kagera Nansio Mwalimu Wa Shule Ya Msingi  Namabugo, Uchunguzi Wa Awali Unaonesha Mwalimu Huyo Kuhusika Na Mauaji Hayo.

Tukio La Tatu; Tarehe 7/9/2019 Huko Wilaya Ya Sengerema  Katika Ufuatiliaji Walikamatwa Watuhumiwa Wanne Kuhusiana Na Tukio La Kuvunja Nyumba Usiku Na Kuiba Silaha Aina Ya Rifle Lililotokea Tarehe 02/09/2019 Huko Kijiji Cha Isaka Kata Ya Nyehunge, Nyg/ir/95/2019 

Silaha Hiyo Imekamatwa Na  Watuhumiwa Wafuatao Wanahojiwa Ambao Ni 1.james S/o Juma 20yrs,msukuma,mkulima Wa Nyehunge Ambao Walikiri Kuhusika Katika Tukio Hilo, 2.alex S/o Panda 49yrs Mnyiramba Mkulima Mkristo Mkazi Wa Isaka Nyehunge, 3.shabani S/o Mohamed 42yrs Mnyamwezi Mkazi Wa Isaka Nyehunge 4.mapambano S/o Charles 35yrs Msukuma Mkulima Mkazi Wa Isaka Nyehunge. 

Baada Ya Kuwakamata Watuhumiwa Waliwapeleka Askari Katika Eneo La Isaka Nyehunge Na Kupelekea Kupatikana Kwa Silaha Rifle Yenye Namba  A 6986 Ambayo Ni Kilelezo Kilicho Ibiwa Katika Tukio Tajwa.

Tukio La Nne; Tarehe 15/08/2019 18:28hrs Huko Mahina Martha D/o Joseph 16yrs , Mnyiramba,  Mwanafunzi Wa Darasa La Sita Shule Ya Msingi Mahina Alikutwa Ameuawa Baada Ya Kubakwa Na Kisha Mwili Wake Kutelekezwa Sehemu Yenye Mawe Mengi. 

Watuhumiwa Wafuatao Wamekamatwa Na Kukiri Kuhusika Na Mauaji Hayo 1. Sospeter S/o Kazumari @babawakuru 37yrs Mkulima Na Mkazi Wa Mwananchi 2. Jastine S/o John @bita 24yrs Mjita Mkulima Mkazi Wa Mwananchi 3.amos S/o Andrea@kilogi 36yrs Mzanaki Fundi Ujenzi Mkazi Wa Mwananchi Na Rebeka D/o Bukindu 35yrs, Msukuma Mkulima Na Mkazi Wa Mwananchi.

Vita Dhidi Ya Madawa Ya Kulevya
Tarehe 04 Hadi 09/09/2019 Katika Wilaya Ya Ilemela Jeshi La Polisi Limefanikiwa Kuwakamata Elizabeth D/o Lucas 53yrs Mkazi Wa Bugando Mission Pamaja Na Hamza S/o Haruna @riko Kwa Tuhuma Za Kujihusisha Na Biasha Ya Madawa Ya Kulevya Wakiwa Na Gram  10 Za Heroine .

Pia Jeshi La Polisi Limefanikiwa Kuwakamata Hellena D/o Nagambona 55yrs Mkerewe Mkazi Wa Mwinuko, Yahaya S/o Haruna 58yrs Mkazi Wa Mwanuko, Shabani S/o Said@ibrahimu 22yrs Mkazi Wa Mwaunuko, Nestory S/o Moses 30yrs Msukuma Na Zainabu D/o Zakaria 45yrs Mwikizu Wakazi Wa Iseni  Wakiwa Bangi Kilo 30 Na Puli 58

Imetolewa Na;
Muliro J. Muliro- ACP
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527