RAIS MAGUFULI ATEUA BOSI MPYA WA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)


Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT. Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Akiba.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo  wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam .

Awali Aprili13, Rais Magufuli alimpandisha cheo Brigedia Jenerali Mbuge kutoka kuwa Luteni Kanali na kuwa Brigedia Jenerali.

Dk. Magufuli alimpandisha cheo hicho Brigedia Jenerali Mbuge baada ya kufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwamo ujenzi wa ukuta wa Mirerani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527