SERIKALI YATARAJIA KUMWAGA TSH.BILIONI 33.5 KWA AJILI YA UJENZI WA WODI 2 KILA HOSPITALI 67 ZA WILAYA NCHINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 10, 2019

SERIKALI YATARAJIA KUMWAGA TSH.BILIONI 33.5 KWA AJILI YA UJENZI WA WODI 2 KILA HOSPITALI 67 ZA WILAYA NCHINI

  Malunde       Tuesday, September 10, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Serikali inatarajia kutoa jumla ya Shilingi bilioni 33.5 kwa ajili ya kujenga wodi 2  katika kila hospitali 67 za  wilaya zinaoendelea kujengwa nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa SELEMANI JAFO  amesema hayo  wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa katika kijiji cha Mlowa Barabarani.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo waziri JAFO amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwahimiza kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru serikali kwa kuimarisha huduma za afya katika mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake mkurugenzi wa CHamwino ATHUMANI MASASI amesema Ujenzi huo ulianza februari mwaka huu kwa kupokea kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na unatarajiwa kukamilika septemba 30 mwaka huu.

Ujenzi wa hospitali hizo ulihusisha jengo la maabara,jengo la wagonjwa kutoka nje,jengo la kuhifadhi dawa,jengo la mama na mtoto,utawala,jengo la mionzi na la kufulia nguo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post