FUNDI UMEME MBARONI KWA KUKUTWA NA SARE ZA JESHI LA POLISI

Fundi umeme aliyekutwa na sare za jeshi la polisi

Na Esther Macha - Malunde 1 blog Mbeya 
Jeshi  la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia fundi umeme, Kelvin Manyusi(32) mkazi wa Teku mkoani hapa akiwa na sare za Jeshi la Polisi ambazo ni TT 2 kitengo cha FFU, koti la mvua rangi nyeusi pamoja na mkanda wa filimbi ambavyo ni mali za Jeshi la Polisi Tanzania.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ulrich Matei alisema mtuhumiwa alikamatwa Septemba 20, 2019 majira ya saa 5:30 alasiri katika msako uliofanyika huko Mtaa wa Ngosi, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya.

Matei alisema mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na vifaa vya kuvunjia ambavyo ni panga, bisibisi pamoja na tindo. 

Alisema kuwa mtuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali mbalimbali zinazodhaniwa ni kuwa ni za wizi. 

Hata hivyo Kamanda Matei alisema upelelezi wa tukio hill unaendelea.
.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527