UZINDUZI WA MBIO ZA ROCK MARATHON 2019 WAFANYIKA MWANZA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 19, 2019

UZINDUZI WA MBIO ZA ROCK MARATHON 2019 WAFANYIKA MWANZA

  Malunde       Thursday, September 19, 2019

Na Fabian Fanuel - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi leo amezindua mbio ndefu za Rock City Marathon 2019 katika Uwanja wa Rock City Mall Mwanza.

Uzinduzi huo umefanyika leo Alhamis Septemba 19,2019 ukishirikisha wadau mbalimbali wa mbio hizo, viongozi kutoka Serikalini, Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Wadhamini wa mbio pamoja na waandishi wa habari.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana  Dkt. Phillis Nyimbi amewashukuru waandaji wa mbio hizo 'Capital Plus International' kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuomba washiriki wengi kujiandisha kwa mwaka huu kushiriki mbio hizo zitakazofanyika Mkoani Mwanza 20 Oktoba mwaka huu.

Huu ni msimu wa kumi wa mbio hizi ambazo zimekuwa na mwitikio mkubwa kutokana na washiriki wengi kuongezeka kila mwaka na mwaka huu inatarajiwa washiriki zaidi ya elfu tatu watashiriki huku waandaji wakiweka bayana zawadi zaidi ya Milioni 30 zitashindaniwa kwa mbio za Aina mbalimbali Kama kilomita 42, 21, 5 na 2.5.

Miongoni mwa wadhamini wa mbio ndefu za Rock City Marathon 2019 ni Tigo Rock City Mall,Tiper, Global Guard,Mwanza Water,Pigeon Hotel,Bodi ya Utalii na Pepsi.
Mkuu wa Mkoa wa Nyamagana Dr Phillis Nyimbi akisaini namba yake ya ushiriki wa mbio za Rock City Marathon huku Mratibu wa mbio hizo Magdalena Laizer na Katibu wa chama cha mbio Mkoa wa Mwanza Peter Mugaya wakishuhudia.


Msimamizi wa Mbio za Rock City Marathon John Bayo akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi medali.
Msimamizi wa Mbio za Rock City Marathon John Bayo akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi medali.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi akionesha medali.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi akionesha medali.

Mkuu w Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi akikata utepe wa Uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon 2019 uliofanyia Viwanja vya Rock City Mall Mwanza.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post