BABU WA MIAKA 81 AFANYIWA SHEREHE BAADA YA KUPOTEA MIAKA 51


Mzee Francis Muthua Chege.
Mzee wa miaka 81 aitwaye Francis Muthua Chege, amerudi nyumbani baada ya kupotea kwa miaka 51 akiwaacha mke wake na watoto sita katika kijiji cha Ikumbi nchini Kenya.

Mzee huyo aliiacha familia yake mwaka 1968 wakati huo akiwa ana umri wa miaka 30 na kutokomea katika misitu ya Mau, ila hakumwambia mke wake na watoto wapi anaelekea.

Baada ya kurudi nyumbani Mzee huyo aliwasimulia watu, ndugu, jamaa na marafiki vitu alivyokuwa anafanya baada ya kutoweka kwa miaka 51.

"Nilikuwa nauza mkaa kisha fedha zote ambazo napata zinatumika kununua pombe. Mke wangu wa pili na mtoto wetu wa kiume walishindwa kuvumilia tabia yangu na wakaamua kuondoka. Niliishi katika masikitiko makubwa na hata kuhofia kurejea nyumbani mikono mitupu," amesimulia Francis Muthua Chege.

Ameongeza kusema alikuwa hana hata nauli ya kurudi kijijini kwao ndipo alipoenda katika kituo cha polisi kuomba msaada kupata nauli kurudi kijijini alipotoka.

Baada ya kurejea kijijini kwao wanafamilia waliandaa karamu fupi ya chakula na vinywaji wakisheherekea tukio la kurudi kwake baada ya muda mrefu.

Source By Nairobi News.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527