RAIS MAGUFULI AMEMSAMEHE JANUARY MAKAMBA NANGELEJA KWA KUMTUKANA KWENYE SIMU

Unazikumbuka zile sauti za vigogo wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizokuwa zinasambaa mitandaoni? Kama unakumbuka basi sikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka kuhusu hizo sauti.


Akizungumza leo na wataalamu wa ujenzi nchini, Rais Magufuli amesema sauti hizo kwa zaidi ya asilimia 100  zilikuwa za kweli na alipofikiria kama suala hilo litakwenda katika kamati ya maadili ya CCM  hali ingekuwa mbaya kwao.

“Nakumbuka hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa. Walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni kweli ni sauti zao lakini nimewasamehe.

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha nikawa najiuliza mimi kila siku naomba msamaha kwa Mungu na ile sala tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe.... nikasema nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa sana watu hao ni January Makamba na Wiliam Ngeleja nikaona niwasamehe tu.

“Waliomba msamaha nikasema ni vijana  na nimewasamehe. Kama palikuwa na mambo mambo mabaya nyuma tuyasahau ili tukaanze upya maana kusamehe siyo jambo rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe,” amesema Rais Magufuli. 

Aliongeza, “Hawa waliokuja kuniomba msamaha mheshimiwa Makamba na Ngeleja niliamua kuwasamehe. Waliomba msamaha, wakanigusa, nikasamehe na kusahau.”

“Kwa hiyo suala la kusamehe ni muhimu, hata akikuudhi, akikutukana namna gani na hata akifanya kazi vibaya akaja kukuomba msamaha namna gani.”


Baada ya kueleza kwa ufupi kuhusu sauti hizo, Rais Magufuli akasita kidogo kuendelea kuzungumza kisha akacheka, “nikasema hawa wakipelekwa katika kamati ya maadili (ya CCM) adhabu itakuwa kubwa.”

Rais Magufuli alikuwa anazungumza katika mkutano wa siku mbili ulioanza leo Dar es Salaam unaohusisha Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB),  Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).

SOMA ZAIDI <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post