KUTANA NA MBWA WA AJABU HAWANA MANYOYA WANAITWA 'MASHETANI' AU 'MBWA WASHAMBA'


Jina la Sumac linamaanisha"kitu kizuri" kwa lugha ya kinyumbani ya Peru, lakini ni bayana kuwa jina hilo halikaribiani na uzuri: kwa vyovyote.

Ni mbwa anayefahamika kama "perro peruano sin pelo", asiye na manyoya kama mbwa wa kawaida mwenye ngozi iliyokunjana .

Yeye na rafiki yake mwingine anajulikana kama , Munay, inayomaanisha "kupendwa na kila mtu ", hutumia muda wao mwingi kuzurura katika milima ya jadi ya Huaca Pucllana mjini Lima.

Hii ni kwa sababu miongo kadhaa iliopita kizazi cha mbwa hao kilikabiliwa na tisho la kuangamia.

Lakini mwaka 2000 serikali ya Peru iliwatambua mbwa hao wenye ''upara'' kama sehemu ya utamaduni wa taifa hilo.

Mwaka mmoja baadae ilitangaza angalau mmoja kati ya mbwa hao wataishi katika makazi ya kiakiolojia yaliopo pwani ya Peru.

Lengo alisema, mwanaakiolojia wa Huaca Pucllana, Mirella Ganoza, ni kudumisha sehemu ya utamaduni wa kale wa Waperu ili usitoweke kabisa.

"Kile tulichogundua ni kwamba tuna kitu ambacho ni chetu," alisema. "Ni ishara ya utambulisho wetu."Mbwa hawa hawakujaaliwa na manyoya mengi katika ngozi yao kama mbwa wa kawaida

'Viumbe wa kishetani'

Mbwa kama Sumac na Munay mara kwa mara huwekwa kwenye michoro ya kipekee ya utamaduni wa jamii ya Inca, Moche, Wari na Chimu cultures, kuashiria kuwa wao ni mabingwa.

Wafugaji wao huwaita "mbwa washamba" kwa sababu ni wachache na kizazi chao hakijawahi kubadilika licha ya kuwa duniani kwa maelfu ya miaka.

Mfugaji mmoja aliongezea kuwa mbwa hao ni muhimu "kama Machu Picchu" katika utamaduni wa Waperu.

Walikua maarufu sana wakati walowezi wa Kihispania walipofika pwani ya Peru mwaka 1532 kabla ya wahispania hao kufuta utamaduni huo na Ukatoki.

Walipowaona mbwa hao wasio na manyoya walisema wana sura mbaya na ya kunatisha- na kwamba wanastahili kuangamizwa.Sumac na Munay wanafikiria ni mbwa wazuri wanaostahili kutunzwa

"Wahispania walihisi ni ''mashetani'' na hivyo ndivyo walivyo tambuliwa na waumini wa Kanisa Katoliki ," Bi. Ganoza anasema. 

"Waliamini mbwa hao walikuwa viumbe wa kiajabu kutokana na muonekano wao wa kustaajabisha."

Baada ya karne kadhaa mbwa hao walianza kutoweka, wengine walifariki na kizazi cha sasa cha jamii ya Peru hakina historia yao.

Wachache waliosalia wamekuwa mbwa wa kuranda randa wasio na wenyewe huku wengine wao wakitelekezwa.

Bi Ganoza anakumbuka alipokua mdogo aliambiwa ni "perros chinos", mbwa wa kichina walioletwa na wimbi la wahamiaji katika karne ya 19 na 20.
Mambo yalibadilika

Lakini mbwa hao walianza kuhifadhiwa miaka ya 1990 na vugu vugu la wanaharakati wa kitamaduni na hatimae mbwa hao ''perros peruanos sin pelo'' walianza walianza kufugwa manyumbani hali iliyofanya waanze tena kukubalika katika jamii.Sumac amekuwa akipendelea sana kuzurura katika maeneo ya kiakiolojia

Wakati serikali ya Peru ilipoidhinisha sheria ya kuwa mbwa kama Sumac na Munay waishi katika makavazi ya kitaifa ya akiolojia maisha yao yalibadilika kabisa.

Hadi wa leo mbwa hao wanaenziwa sana kote nchini Peru.

Nchi hiyo imebuni kamati ya kitaifa ya kulinda mbwa hao wa kipekee na iliyopendekeza kila tarehe 12 mwezi Juni- iwe siku ya kitaifa yakusherehekea mbwa wa Kiperu wasio na manyoya.

Sumac na Munay wanatumiwa kama kivutio cha wataliiHistoria ya mbegu ya Sumac na Munay ni sehemu ya maelekezo kwa watalii wanaozuru nchi ya Peru
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527