WAANDISHI WA HABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA HABARI ZENYE KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 20, 2019

WAANDISHI WA HABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA HABARI ZENYE KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA

  Malunde       Friday, September 20, 2019

Waandishi wa habari hapa nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuandika habari zenye upande wa jinsia moja, bali waandike habari ambazo zitakuwa na usawa wa jinsia zote ili kutoa fursa ya kupaza sauti kwa wote.Rai hiyo imetolewa  leo, Septemba 20, 2019  na  Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMMWA),Joyce Shebe kwenye mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, juu ya kuandika habari za kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kugombea nafasi za uongozi ikiwemo siasa, yanayo endeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP 'TGNP Mtandao'

Akiwasilisha mada namna ya kuandika habari zenye mrengo wa kijinsia, Shebe amesema waandishi wa habari wanapokuwa wakiandika habari zao wazingatie usawa wa Kijinsia.

Amesema katika habari nyingi ambazo zimekuwa zikiandikwa Jinsia ya kike imekuwa haipewi kipaumbele sana tofauti na ya kiume, na hivyo kuwafanya kushindwa kupaza sauti zao na kukwamisha utatuzi wa matatizo yao.

“Waandishi wa habari mnapokuwa mnaandika habari zenu, zingatieni pia kubalance Jinsia zote na kuacha kuandika habari za Single Source, bali changanyeni jinsia zote ili kila mmoja aweze kupata fursa ya kupaza sauti, na kuelezea changamoto zao na kuweza kutatuliwa,”amesema Shebe.

“Pia katika habari hizo msitumie lugha ambazo zitaikwaza Jinsia nyingine, bali ziwe nzuri na zisizo leta ukatili, mfano kwenye chombo kimoja cha habari katika matokeo ya mtihani la saba, waliandika mwanafunzi aliyekataliwa na baba yake ameongoza mtihani, hii lugha siyo rafiki ambapo inaumiza upande mmoja wa jinsia,”ameongeza.

Mafunzo hayo yaliyoshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro, Mara, Geita, Rukwa, Pwani, pamoja na Shinyanga,yanafanyika kwa muda wa siku tatu, kwenye Hotel ya Silver Paradise Jijini Dar es salaam, na leo ni siku ya pili ambapo yatahitimishwa kesho Jumamosi Septemba 21,2019.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwezeshaji Joyce Shebe akitoa mada kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari zenye mrengo wa kuzingatia usawa wa kijinsia. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Waandishi wa habari wakisikiliza mada namna ya kuandika habari zenye mrengo wa kuzingaitia usawa wa kijinsia.

Mwandishi wa habari Remmy Maliva kutoka Ndingala Radio akichangia mada kwenye mafunzo.

Mwandishi wa Gazeti la Nipashe Mkoani Morogoro Christina Haule akichangia mada kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya makundi wakiangalia namna Magazeti yanavyo andika habari kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mwandishi wa habari Eva Lucas kutoka Huheso Radio wilayani Kahama Mkoani Shinyanga akiwasilisha kazi ya kikundi namna walivyoangalia Magazeti yanavyoandika habari kwa kuzingatia usawa wa Kijinsia.

Mwandishi wa Habari Bahati Mustapher ambaye ni mwenyeti wa Kilimanjaro Press Club akiwasilisha kazi ya kikundi namna walivyo angalia Magazeti yanavyoanidika habari kwa kuzingatia usawa wa Kijinsia.

Mwandishi wa habari Costancia Michael kutoka Top Radio mkoani Morogoro akiwasilisha kazi ya kundi namna walivyo angalia Magazeti yanavyo andika habari kwa kuzingatia usawa wa Kijinsia.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post