LOWASSA : 'KAZI ZA RAIS MAGUFULI ZINAPASWA KUPAKWA 'PODA'...NCHI IMEWAKA MOTO"

 Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuondolewa kazini kwa watendaji wazembe na wasiotimiza wajibu wao umefanya nchi kushika adabu.

Lowassa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 20, 2019 katika mahafali ya Shule ya Msingi Meyers Jijini Arusha.

"Rais Magufuli (John) anastahili pongezi anafanya kazi nzuri sana, tunaona mawaziri wanafanya kazi nzuri ,Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo kule wengine huku nchi imewaka moto kila sehemu,” amesema.

Asema kazi nzuri za Rais zinapaswa kupakwa ‘poda’ kwa kuhusisha na kuboresha elimu ambayo itawapa ujuzi wahitimu kujiajiri.

"Kuna vijana wengi wanamaliza masomo kutokana na mpango wa elimu bure sasa tujitahidi elimu hii iwasaidie vijana kupata ujuzi na ubunifu ili kuweza kujiajiri" amesema Lowassa.

Via >>Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527