KUTANA NA MJUSI MKUBWA KULIKO WOTE AGUNDULIWA

Giant salamander: Not one species but three

Aina mpya ya mjusi imegundulika na kudhaniwa kuwa ndiye mjusi mkubwa zaidi duniani, kwa mujibu wa vithibitisho vya vina saba vilivyotolewa na makumbusho ya wanyama.

Amphibia huyo mwenye muonekano wa mjusi ana upana wa mita mbili na anapatikana kusini mwa China.

Mjusi huyo mkubwa amekuwa ni miongoni mwa wanyama wa pori wanaogopwa zaidi.

Wanasayansi wanasema kwamba watu wa hifadhi ya wanyama wanapaswa kufanya jitihada za kumuokoa mjusi huyo au atapotea.

Mwanzoni, mjusi huyo mkubwa alidhani kuwa ndiye peke yake ambaye ana ukubwa kiasi hicho.

Lakini utafiti unaonyesha kuwa wapo amphibia watatu wa aina hiyo katika maeneo mbalimbali nchini China.

Ingawa amphibia aliyepatikana Kusini mwa China , ndio mjusi mkubwa zaidi kati ya hao watatu.

Hata hivyo watafiti wanadhani kuwa huyo ndio amphibia pekee mkubwa ambaye yuko hai.

Profesa Samuel Turvey kutoka jumuiya ya wataalamu wa Zoolojia mjini London anasema kuwa idadi ya wanyama pori imeongezeka kwa kasi.Mjusi aliyehifadhiwa katika makumbusho ya London tangu mwaka 1920

"Tuna imani kuwa kutakuwa na ueleo mpya wa kuhifadhi wanyama na hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda uepo wa viumbe hai hao" Mtafiti alisema

"Utafiti huu unakuja wakati ambao China inapaswa kuwalinda amphibia wakubwa walioko porini," Melissa Marr,mtafiti wa masuala ya kihistoria.

Mijusi mikubwa ilionekana katikati ya nchi hiyo, mashariki na kusini mwa China.

Miaka ya hivi karibuni, soko la vyakula vya starehe limeongezeka nchini humo hivyo kufanya idadi ya uwindaji wa wanyama pori kuongezeka pia.

Utafiti umebaini nini katika mjusi?

Wanasayansi walitumia viumbe hai ambavyo vina muonekano sawa na mjusi mkubwa anayepatikana China, na kuangalia asili ya mnyama huyo ni wapi..

Wazo lilikuwa ni kuona kama mjusi wa China ana utofauti na mjusi mkubwa aliyedaiwa kuwa mkubwa mwaka 1920 ambaye amehifadhiwa Uingereza.

Walitaka kujua kama ana tabia sawa na mjusi huyo mpya.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527