AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIDAI BUKU JERO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 17, 2019

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIDAI BUKU JERO

  Malunde       Tuesday, September 17, 2019
Mtu mmoja aitwaye Rajabu Abdalah amefariki dunia kwa kuchomwa kisu baada ya kudai 1500 kama malipo yake.

Mtu huyo  amefariki dunia katika tukio hilo lililofanyika Kata ya Babati wilaya ya Babati mkoani Manyara, baada ya mwenzake kumchoma kisu chini ya titi la upande wa kushoto wakiwa wanagombania shilingi 1500.

Imeelezwa kuwa kiasi hicho cha fedha walipewa na abiria kama malipo baada ya kumbebea mzigo wake kuupeleka katika stendi ya magari.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga, amesema kuwa kutokana na opereseheni kubwa iliyofanyika kumsaka kijana Cleophace John a.k.a Mgogo aliyefanya mauaji hayo walifanikiwa kumpata.

''Tumefanya msako mkubwa na kumkamata mtuhumiwa aitwaye Cleophace John au maarufu Mgogo, akiwa ndani ya gari aina ya Emmigrace leo Asubuhi ya Septemba 17, 2019 akiwa anajaribu kutoroka kuelekea jiji la Dodoma'', ameeleza RPC. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mji Mrara, ukisubiri uchunguzi wa daktari, huku mtuhumiwa akiwa mikononi mwa polisi kwa mahojiano zaidi.
Via >> EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post