MBUNGE HALIMA BULEMBO AKERWA FIGISU FIGISU UTOAJI MIKOPO KWA AKINA MAMA NA VIJANA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera ,Mhe. Halima Abdallah  Bulembo

Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Vijana mkoani Kagera wametakiwa kuzitolea taarifa halmshauri zote za mkoa huo mbazo zinakwama kutoa mikopo kwa vijana,watu wenye ulemavu na wanawake.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 17, 2019 na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera ,Mhe. Halima Abdallah  Bulembo wakati akizunguza kwenye uzinduzi wa Misenyi ya kijani iliyofanyika wilayani humo. 

Mbunge huyo amewataka vijana kuzitolea taarifa halmashauri ambazo hazitoi mikopo kwa kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha maendeleo ya kundi hilo nyuma na taifa kwa ujumla. 

Bulembo amesema amebaini suala la utoaji mikopo kwa vijana na akina mama kuonekana kusuasua hivyo kusisitiza mikopo itoke ili vijana wajiajiri ili kuliendeleza taifa lenye maendeleo

"Mara utaambiwa kikundi hiki hakijitoshelezi,mara umezidi umri,figisu figisu za nini? Nawaambia vijana wenzangu jiamini mikopo ni haki yenu hamfanyiwi hisani mnatakiwa kukopeshwa,’’amesema.

Hata hiyo ametoa wito kwa vijana katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uchaguzi na kuacha kulalamika badala yake wafanye shughuli za maendeleo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kagera ,Mhe. Halima Abdallah  Bulembo 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527