MBUNGE MGIMWA KUTATUA TATIZO LA BARABARA YA MTILI,IFWAGI,LULANDA MPAKA MPANGATAZARA


Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea wa kijiji cha Ibwanzi kilichopo kata ya Ihanu akielezea jinsi ya kutatua changamoto ya barabara kwa kuwa ashapata fedha za kutatulia kero hiyo inayokwamisha maendeleo ya tarafa ya Ifwagi.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa anakagua barabara ya kutoka Mtili hadi Mpangatazara.
Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi akielezea jinsi ambazo watatengeneza barabara ya Mtili hadi Mpangatazara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi ubovu wa daraja la Nandala
***
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini kutatua changamoto ya barabara kwa wananchi wa tarafa ya Ifwagi kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu kwa kuwa changamoto hiyo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kwa wananchi wa tarafa hiyo.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara ya kata za Mpangatazara,Ihanu na Ifwagi mbunge Mahmoud Mgimwa alisema kuwa changamoto ya barabara imekuwa kero kwa kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya wananchi wa tarafa ya Iwagi.

“Kweli hata mimi nimekuwa nikiiona changamoto hii na imekuwa inaninyima usingizi mara kwa mara kwa kuwa inakwamisha maendeleo ya wananchi kwa kuwa shughuli nyingi za kimaendelo zimekuwa zinategemea barabara kwa kiasi kikubwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wamepata kiasia cha shilingi milioni mia tisa ishirini na moja kwa ajili ya kutengeneza barabara ya kutoka Mtili,Ifwagi,Lulanda hadi Mpangatazara kwa kiwango cha changarawe ili kutatua tatizo hilo kwa muda mrefu.

“Jamani msione nilikuwa sionekani wala siji kwenye mikutano ya hadhara kwa sasbabu barabara hii ilikuwa inaniumiza kichwa ila kwa sasa nakuja kifua mbele na kiburi kwa kuwa tayari fedha nimetafuta na nimewapa hawa TARURA kwa ajili ya kutengeneza barabara hii” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kiwango bora ambacho kinaweza kudumu kwa miaka mitano bili kuharibia kwa kiasi kikubwa bali kutakuwa na matengenezo madogo madogo ambayo hayaepukiki.

Aidha Mgimwa amewataka wananchi ambao wanapitiwa na barabara hiyo kuakikisha kuwa barabara hiyo inatengenezwa kwa kiwango kulingana na gharama ambazo wamezitoa kwa kuwa fedha inayotumika hapo ni kodi ya wananchi na wao ndio wenye mali hiyo.

“Barabara hii ikianza kutengenezwa ni jukumu letu sote kuhakikisha inatengenezwa kulingana na michoro iliyopo kwa mujibu wa mkataba la sivyo wasiipokee barabara hiyo ikikamili,mkipokea barabara ambayo ipo chini ya kiwango hilo litakuwa sio jukumu langu kwa kuwa wajibu wa kutafuta fedha mimi kama mbunge nimeshalifanya” alisema Mgimwa

Kwa upande wake kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi alikiri kwenye mikutano ya hadhara kupokea fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe.

“Ni kweli mbunge wenu ametafuta fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hii milioni mia tisa ishirini na moja na tayari zipo benk kwenye akaunti zetu na tunarajia kuanza kuzitumia hivi karibu kwa lengo la kutatua changamoto hii ambao imekuwa kero kwenu” alisema Mjohi

Mjohi aliongeza kuwa tayari walishatangaza zabuni na wameshawapata wakandarasi wawili ambao watahusika kutengeneza barabara hiyo kwa kuwagawana kimeta ambazo zipo kwenye barabara hiyo.

“Niwatoe hofu kuwa wakandarasi wataanza kazi mapema mwezi wa kumi mwaka huu kutengeneza barabara yetu kwa kuwa mwezi huu watasaini mikataba ya kuanza kazi na watapita kila kijiji kutoa taarifa kuwa wanaanza kazi ya ujenzi wa barabara hizo” alisema Mjohi

Mjohi aliungana na mbunge wa jimbo hilo Mahmoud Mgimwa kwa kuwataka wananchi kusimamia utengenezwaji wa barabara hiyo kulingana na michoro watakayo pelekewa ili kuhakikisha ubora wa kutengeza barabara hiyo unazingatiwa na ni jukumu lao.

“Nao baadhi ya wananchi walimpongeza mbunge huyo kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha analeta maendeleo kwenye jimbo hilo na kusema kuwa wanamshukuru endapo barabara hizo zitakamilika kutengenezwa” walisema wananchi



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527