WANANCHI WATAKIWA KULINDA VYANZO VYA MAJI ZIWA VICTORIA



Afisa Maji Kupitia Ofisi Ndogo ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Mberwa Olengeire 

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Afisa Maji Kupitia Ofisi Ndogo ya Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Mberwa Olengeire amewataka wananchi kuhifadhi ,kulinda na kuthibiti uchafuzi katika vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa matumizi endelevu.

Olengeire ametoa rai hiyo Septemba 18,2019 wakati akiongea na vyombo vya Habari ofisini kwake ambapo amesema licha ya elimu kuendelea kutolewa wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakifanya kuvunja sheria na kanuni katika kulinda,kutunza na kuhifadhi vyanzo hivyo kwa maksudi huku wakijua kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Amesema uwepo wa vyanzo vya maji vilivyo salama husaidia miradi ya kusambaza maji kuwa yenye mafanikio makubwa.

‘’Tuungane na Rais wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli katika kuelekeza Tanzania ya Viwanda kwa kuvitunza na kuvilinda nyanzo vya maji Ziwa Victoria kwani ndiyo uchumi wetu,kwa hiyo atakayekiuka maagizo ya viongozi wa nchi yetu atafikishwa katika vyombo vya dola’’alisema..

Afisa huyo amesema kila mtu anapaswa kumlinda mhusika yeyote anayeharibu chanzo cha maji na kutoa taarifa ili awajibishwe vilivyo na kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kulima karibu na vyanzo vya maji, kukata miti ambayo ni rafiki wa vyanzo vya maji, kutopanda miti isiyo rafiki na maji katika vyanzo hivyo kwani shughuli hizo ni vinaharibu wa vyanzo vya maji. 

Amesema elimu itaendelea kutolewa na kuwa watakaokaidi watapelekwa mahakamani au kutozwa faini huku akiitaka jamii kushirikiana na bodi za mazingira katika uhifadhi wa mazingira kutunza na kuviendeleza vyanzo vya maji vilivyopo.

Amesema Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ni Taasisi inayoshughulika na usimamizi wa rasilimali za maji ikiwemo kulinda na kuthibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji katika bonde la Ziwa Victoria na eneo lote muelekeo wa maji ambayo uingia katika ziwa Victoria ambapo ametaja Bonde la ziwa Victoria kuigusa mikoa 5 ikiwemo ni Mara , Mwanza , Simiyu ,Kagera Na Shinyanga.

Aidha Olengeire  amesema jamii itambue sekta ya maji kuwa ni sehemu muhimu hivyo ni vyema kulinda vyanzo hivyo na kuvitunza kwa kuzuia ukataji miti, kulima kwenye vyanzo vya maji, pamoja na shughuli zote ambazo haziruhusiwi kufanyika ndani ya mita 60.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527