TETESI ZA SOKA LEO ALHAMIS SEPTEMBA 19,2019 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 19, 2019

TETESI ZA SOKA LEO ALHAMIS SEPTEMBA 19,2019

  Malunde       Thursday, September 19, 2019
Manchester United inatumai kumshawishi mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba kusaini mkataba mpya. Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kiungo cha mbele wa miaka 17 anayeichezea timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Mason Greenwood pia wameorodheshwa kwa mikataba mipya. (Standard)

Mashabiki wenye hasira wa Real Madrid wametaka Zinedine Zidane afutwe kazi kama meneja wa timu hyo baada ya Paris St-Germain kuitandika kichapo katika mechi ya ligi ya mabingwa (Sun)

Juventus imekataa fursa ya kumsajili Dani Alves msimu huu wa joto kabla ya mlinzi huyo mwenye miaka 36 kujiunga na Sao Paulo katika uhamisho wa bure. (Calciomercato)

Manchester United imetuma wakala kwenda kumtazama mchezaji wa kiungo cha mbele wa Norway Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 19, wakati akijitambulisha katika jukwa la Ulaya kwa kuifungia Red Bull Salzburg katika mechi yake ya kwanza katika ligi ya mabingwa . (Salzburger Nachrichten, kupitia Sport Witness)

Blackburn inafanya mazungumzo kumsajili aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham na Fulham Lewis Holtby, raia huyo wa Ujerumani mwenye miaka 29 ambaye amekuwa wakala wa bure tangu aondoke Hamburg msimu uliopita. (Mail)
Everton ina hamu ya kumsajili mshambuliaji mwenye umri wamiaka 19 wa Ireland kaskazini David Parkhouse, ambaye kwa sasa amechukuliwa kwa mkopo na Derry City kutoka Sheffield United. (Football Insider)

Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, anafikiria kustaafu kutoka soka ya kimataifa na Ujerumani baada ya mashindano ya ubingwa mwaka ujao. (Bild)

Winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 Jadon Sancho, anayelengwa na Manchester United amekataa kuthibitisha kutoondoka kutoka klabu hiyo msimu ujao wa majira ya joto. (Viasport, kupitia Metro)

Manchester United inaiangalia hali ya Thomas Tuchel akiwa huko Paris St-Germain iwapo wataamua kuijaza nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer. (Le10 Sport, kupitia Sport Witness)

Mlinzi Virgil van Dijk, mwenye miaka 28, amepuuzia pendekezo kuwa anakaribia kukubali mkataba mpya na Liverpool. (Sky Sports, kupitia Mail)
Chelsea imefungua mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha mbele Tammy Abraham na mlinzi Fikayo Tomori kuwapatia wachezaji hao wa timu ya taifa ya England mikataba ya miaka mitano kila mmoja. (Guardian)

Tottenham inafikiria iwapo kumrudisha winga Jack Clarke kutoka uhamisho wake wa mkopo huko Leeds huku mchezaji huyo wa miaka 19 akitarajiwa kushiriki mechi ya ligi msimu huu. (Mail)

Uefa itathibitisha uga wa Wembley kuwa mwenyeji wa mashindano ya fainali ya ligi ya mabingwa 2023 wiki ijayo. (Sky Sports)

Arsenal imewasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Hungary mwenye miaka 18 Dominik Szoboszlai kutoka RB Salzburg. (Football.London)
Na meneja wa Gunners, Unai Emery amewapeleka wachezaji wake katika mtoko wa usiku mjini London saa chache baada ya mtanange wao dhidi ya Watford Jumapili. (Mirror)

Mfanyabiashara wa Marekani Dave Checketts na Alan Paceremain wamevutiwa kuinunua Sheffield United iwapo Mwanamfalme Abdullah ataamua kuiuza klabu hiyo ya soka. (Mail)
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post