MBUNGE HALIMA BULEMBO ATOA MSAADA KWA KOMPYUTA NA PRINTER KWA MAKATIBU WA CCM KAGERA

Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Halima Abdallah Bulembo amekabidhi Printer 10 na Kompyuta 10 kwa Makatibu wa CCM wa wilaya 8 za mkoa wa Kagera ili kuunga mkono shughuli za Chama Cha Mapinduzi CCM kufanyika bila vikwazo.


Mhe. Bulembo amekabidhi vifaa hivyo leo Septemba 20,2019 katika ofisi za Chama hicho zilizopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ikiwa ni kuunga mkono shughuli za chama hicho kusonga mbele na kuwezesha wanachama wa chama hicho kutenda kufanya kazi za chama hicho bila kuwa na changamoto.

Akipokea vifaa hivyo,Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndegereki ameahidi kutumia vifaa hivyo vizuri kwa shughuli za chama huku akimpongeza mbunge huyo kwa kuwapatia vifaa hivyo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Halima Abdallah Bulembo akikabidhi Printer 10 na Kompyuta 10







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527