TUNDU LISSU KUTUA BONGO MWEZI UJAO...KATAJA WATU WATAKAOMSINDIKIZA


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema taasisi na watu mbalimbali wamejitokeza kutaka kumsindikiza, pindi atakapotaka kurudi Tanzania, itakapofika mwezi wa 10,2019.

Tundu Lissu ameeleza hayo kupitia andiko lake akieleza miaka 2 ya tangu aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma, na kusema kipindi cha miaka 2 kilikuwa cha kipindi cha mateso na matumaini.

"Kuna wawakilishi wa taasisi za Kidini na Kijamii, ndani na nje ya nchi yetu Wanadiplomasia kutoka nchi rafiki na Mashirika ya Kimataifa, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya Kimataifa, ambao wameonesha nia ya kunisindikiza katika safari yangu ya kurudi nyumbani." ameandika Tundu Lissu.

"Katika mazingira haya, kurudi kwangu nyumbani hakuwezi kufanywa siri ni muhimu, kwa hiyo, tarehe ya kurudi kwangu nyumbani ijulikane wazi kwa kila mtu." ameandika Tundu Lissu.

Awali Lissu alitangaza kurudi nchini Septemba 7, 2019, lakini imeshindikana kwa kile alichokidai kuwa Daktari wake amemtaka kukutana naye mwezi wa 10.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post