KUELEKEA MTIHANI DARASA LA SABA, DED AAGIZA KUVUNJA MAKUNDI YOTE YA WHATSAAP | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 10, 2019

KUELEKEA MTIHANI DARASA LA SABA, DED AAGIZA KUVUNJA MAKUNDI YOTE YA WHATSAAP

  Malunde       Tuesday, September 10, 2019

Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma imevunja makundi yote ya ‘WhatsApp’ ya waratibu elimu msingi ili kuepuka udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba inayofanyika kesho na keshokutwa.

Katika barua hiyo iliyoandikwa kwa waratibu kata elimu wote Agosti 19, 2019 na kusainiwa na Josephat Ambilikile kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo imewataka waratibu elimu kata wote kuvunja makundi hayo.

Makundi hayo ni yale yanayotumika kutoa au kupokea taarifa zozote zinahusiana na utendaji wa taaluma.

Ambilikile amesema pia ofisi imebaini kuwepo kwa makundi ya WhatsApp katika halmashauri hiyo yanayotoa taarifa mbalimbali za kielimu na kijamii.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post