MAHAKAMA YAMTIA HATIANI MCHUNGAJI MWENYE WAKE WATATU


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam  imemuhukumu Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) kulipa faini ya Sh2 milioni au kutumikia kifungo cha miaka miwili.

Wakati huohuo, mahakama hiyo imewahukumu Eather Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) ambao ni wake wa mchungaji huyo na Samwel Samy (22) kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja.

Akitoa Hukumu hiyo leo Jumanne Septemba 10, 2019 Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando amesema baada ya kulipa faini au kutumikia kifungo hicho watuhumiwa hao wanatakiwa kurudishwa nchini kwao.

Wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji Godfley Ngwijo  akisaidiana na Sitta Shija, wakisoma mashtaka kwa nyakati tofauti walidai kwamba, Septemba 2 mwaka huu eneo la Salasala Kilimahewa, Dar es Salaam, mchungaji huyo na wenzake walibainika kuingia nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa mchungaji huyo pekee alibainika  kujihusisha na kazi za kanisa akiwa hana kibali cha makazi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Mchungaji David alikiri shtaka la kwanza la kuingia nchini bila kibali na kukiri shtaka la pili kufanya kazi ya uchungaji huku akiwa hana kibali cha makazi.

Washtakiwa wengine walikiri shtaka la kuingia nchini bila kibali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post