IGP SIRRO APANGUA MAKAMANDA WA POLISI...YUMO WA MOROGORO

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo ya makamanda wa polisi wa mikoa (RPC).



Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Septemba 17, 2019 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, David Misime amesema katika mabadiliko hayo Wilbroad Mutafungwa amehamishiwa makao makuu akitoka Morogoro.

Misime amesema nafasi ya Mutafungwa imechukuliwa na Hamisi Issa aliyekuwa Kilimanjaro. 

Amesema Saidi Hamdani aliyekuwa Njombe amehamishiwa Kilimanjaro na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Geita, Daniel Sillah anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Njombe.

“Mabadiliko haya ni ya kawaida katika kuboresha utendaji kazi wa jeshi la polisi,” amesema Misime

Ingawa Misime amesema mabadiliko hayo ni ya kawaida lakini huenda kwa Kamanda wa Polisi wa Morogoro yamefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Bungeni jijini Dodoma.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527