Serikali Yamwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)..... Yasisitiza Tanzania HATUNA Ugonjwa wa EBOLA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 24, 2019

Serikali Yamwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)..... Yasisitiza Tanzania HATUNA Ugonjwa wa EBOLA

  Malunde       Tuesday, September 24, 2019
Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari. 

Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna Ebola na itashirikiana na Serikali.

Aidha, katika mazungumzo hayo WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu.

Haya yanajiri wakati shirika la madaktari wasio na mipaka Medicins Sans Frontiers MSF limelituhumu shirika la WHO kwa kutumia mfumo usiofaa wa utoaji chanjo nchini DRC  likisema utaratibu wa mgao unaotumika unaruhusu virusi kujitokeza tena katika jamii ambazo tayari ugonjwa huo ulikuwa umetokomezwa na watu kulindwa kutokana na maambukizi mapya.

Shirika la WHO limekanusha madai kwamba linatoa chanjo kwa mgao na badala yake limesema linafanya kazi kwa bidii kama mashirika mengine kuutokomeza kabisa mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo. 


Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba linashirkikiana na serikali ya Congo kuzifikia jamii nyingi na watu wengi kadri inavyowezekana katika maeneo yaliyoathirika na mlipuko wa ebola na wala halijaweka kiwango wala vikwazo katika utoaji wa chanjo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post