Breaking : RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKUU WA MKOA WA MOROGORO..KATEUA VIONGOZI KADHAA...HAYA HAPA MAJINA


Rais John Pombe Magufuli
Zaidi tazama Video hapa chini.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Septemba 20,2019 amemteua Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Lootha Sanare, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Dkt. Steven Kebwe ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Akitangaza uteuzi na utenguzi huo leo Septemba 20, 2019 Katibu mkuu kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, ameeleza kuwa Rais amefanya uteuzi na mabadiliko kadhaa.

Rais  Magufuli pia amefanya uhamisho wa wakuu wa wilaya wawili; Charles Kabeho aliyekuwa Tarime amekwenda Chato na aliyekuwa Chato, Msafiri Simeon amekwenda Tarime.

Ameteua katibu mkuu mmoja, naibu makatibu wakuu watatu na naibu wakili mkuu wa Serikali mmoja.

Pitson Nzunda aliyekuwa naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia masuala ya elimu amekuwa katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge.

Aliyekuwa kamishna wa bajeti katika Wizara ya Fedha, Mary Maganga ameteuliwa kuwa naibu Katibu Mkuu atakayeshughulikia utawala katika wizara hiyo.


Anthony Sanga, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira jijini Mwanza ameteuliwa kuwa naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Dk Ally Posi ameteuliwa kuwa naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye awali alikuwa naibu wakili Mkuu wa Serikali huku nafasi yake ikichukuliwa na Gabriel Malata aliyekuwa kamishna wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Rais pia amewahamisha naibu makatibu wakuu wawili; Nicolas Mkapa aliyekuwa naibu katibu mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuendelea na wadhifa huo huku Mathias Kabudunguru aliyekuwa katika wadhifa huo katika wizara hiyo akipelekwa kuendelea na wadhifa huo wizara ya Tamisemi.

Makatibu Tawala walioteuliwa na maeneo yao katika mabano ni Alphayo Kidata (Mtwara), Emmanuel Kalogero (Morogoro) na Dk Habib Kazungu (Kilimanjaro).


Rais Magufuli pia ameteua mabalozi 12 wakisubiri kupangiwa vituo vyao vya kazi baada ya waliopo katika nchi hizo kustaafu, kurejeshwa nyumbani kupangiwa kazi nyingine.

Walioteuliwa ni Dk Modestus Kipilimba ambaye ni mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa; mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana; aliyekuwa mkaguzi mkuu wa ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga; Jilli Maleko ambaye alikuwa katibu tawala wa mkoa wa Mtwara na Meja Jenerali mstaafu Anselm Bahati.


Wengine ni Profesa Mbena aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha St John’s; katibu mkuu mstaafu Maimuna Tarishi; meja Jenerali mstaafu Gaudence Milanzi; Ali Mwadili aliyekuwa kansela mkuu ubalozi mdogo wa Dudai na Jestus Kinyamwanga, mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje.


Wengine ni Profesa Kennedy Gaston ambaye alikuwa katibu mkuu wa taasisi ya kimataifa ya Asian African Legal Consultative Organization ambayo makao yake makuu yako New Delhi India na Aishi Amour, ambaye alikuwa katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.


Dk Kijazi amevitaja vituo vya kazi vya mabalozi hao kuwa ni Abudhabu Falme za Kiarabu, Bujumbura (Burundi), Bruissels (Ubeligiji), Pretoria (Afrika Kusini), Cairo (Misri), Harare (Zimbabwe), Kuwait City (Kuwait), Riadhi (Saudi Arabia), Tokyo (Japan), Umoja wa Mataifa, Switzerland, Umoja wa Mataifa New York Marekani na Abuja Nigeria.


Rais amewapandisha vyeo maofisa watatu kuwa mabalozi ambao ni Steven Mbungi ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa idara ya ulinzi siasa na usalama Wizara ya Mambo ya Nje ; Ally Bujiku na Dk Mussa Ulandala ambao ni wasaidizi wa Rais.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527