RPC MULIRO AZUNGUMZIA FUJO ZA KLABU ZA SOKA LEO MWANZA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 20, 2019

RPC MULIRO AZUNGUMZIA FUJO ZA KLABU ZA SOKA LEO MWANZA

  Malunde       Friday, September 20, 2019

Kamanda Jumanne Murilo

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Jumanne Murilo amezungumzia juu ya fujo zilizotokea leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza baina ya Kagera Sugar na mashabiki wa timu ya Alliance.

Fujo hizo zilizuka baada ya Kagera Sugar kufanya mazoezi katika Uwanja wa Nyamagana ambao inadaiwa kuwa ulikuwa katika ratiba ya Alliance ambayo leo inatarajia kucheza na Biashara United.

 Kamanda Murilo amesema, "leo ni siku ya mechi kati ya Alliance FC na Biashara United lakini nasikia kuna timu ya Kagera Sugar ipo hapa. Watu wanaofanya mazoezi ni hizi timu mbili zingine, wao Kagera wakaenda mahala hapo kwa hiyo zikafanyika fujo kiasi".

"Nilichokifanya mimi nimeagiza OCD wa pale kufuatilia, hizo taarifa za kocha kuumizwa sijazifahamu. Sisi tunaanzia kuhoji kule kule na kuhusu hili tumeanzia kuhoji kulekule kujua nini shida", ameongeza.

Alliance FC inatarajia kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Biashara United katika Uwanja wa Nyamagana, kesho Kagera Sugar itacheza dhidi ya Mbao FC.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post