MAJERUHI WATATU AJALI YA LORI LA MAFUTA MOROGORO WARUHUSIWA KUTOKA MUHIMBILI


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imethibitisha kuwa, majeruhi watatu kati ya 11 wa ajali ya moto Morogoro waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo, wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya zao kuimarika.

Akizungumza leo Septemba 12, Dkt Edwin Mrema  ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Upasuaji amesema kuwa, kabla ya kuwaruhusu  hospitali hiyo imewapa huduma za kisaikolojia kwa kuwa tatizo la moto lilikuwa limewathiri kwa kiasi kikubwa.

“Majeruhi walikuwa wamebaki 11 hivyo sasa wamebaki wanane kati ya 47 waliofikishwa Muhimbili Agosti 11, ambapo majeruhi 36 walipoteza maisha. Tunaendelea kuwatibu majeruhi na kuwatafuta wanasaikolojia."  Amesema Dk Mrema.

Akizungumzia mgonjwa ambaye hadi sasa yuko kitengo cha uangalizi wa karibu (ICU), amesema kwa kuwa alikuwa ameungua zaidi miguuni, iliwalazimu kutoa viungo ambavyo vilionekana kupoteza uhai na amehifadhiwa katika chumba maalumu cha uangalizi ili kuzuia maambukizi kwa majeraha yake.

Aidha wakati mgonjwa mmoja bado yupo ICU, wengine wapo wodi ya kawaida wakiendelea na matibabu na hali zao zinaimarika.

Tukio la ajali ya moto Mkoani Morogoro, lilitokea Agosti 10, baada ya lori la mafuta kupinduka na kupelekea mlipuko wa moto


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527