BABA LEVO AONGEZEWA KIFUNGO GEREZANI...SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MWAKA 1 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 11, 2019

BABA LEVO AONGEZEWA KIFUNGO GEREZANI...SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MWAKA 1

  Malunde       Wednesday, September 11, 2019

Diwani wa Mwanga Kaskazini(ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Revocatus Chipando maarufu “Baba Levo“ ameongezewa  kifungo Gerezani na sasa atatumikia kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 badala ya Miezi 5 ya awali.


Hukumu hiyo imetolewa jana Septemba 10, 2019 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, baada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali.

Baba Levo alikata rufaa katika mahakama hiyo kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia trafiki, F.8350 PC Msafiri Mponela.

Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post