WAZIRI WA KILIMO AKAGUA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU KUHUSU UNUNUZI WA PAMBA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 8, 2019

WAZIRI WA KILIMO AKAGUA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU KUHUSU UNUNUZI WA PAMBA

  Malunde       Thursday, August 8, 2019
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 6 Agosti 2019 amefanya ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima.

Mhe Hasunga ametembelea na kukagua Kituo cha ununuzi wa Pamba cha Itemelo kilichopo kata ya Dutwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Kituo cha ununuzi cha Lugulu katika kata ya Lugulu Wilaya ya Itilima na Kituo cha Kumalija kilichopo katika kata ya Shanwa wilayani Maswa.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri amejionea hali ya ununuzi wa Pamba ya wakulima ukiwa unaendelea kutokana na serikali hivi karibuni kupata muarobaini wa mustakabali wa zao hilo.

Waziri huyo wa Kilimo amepiga marufuku Pamba ya wakulima kupimwa katika mizani zisizofahamika badala yake lazima ipimwe katika mizani iliyothibitishwa na wakala wa vipimo.

Katika hatua nyingine pia Mhe Hasunga ametoa kalipio Kali kwa wanunuzi wa Pamba kadhalika vyama vya ushirika vinavyowakata kilo moja wakulima kwa madai ya mifuko ya kupimia badala yake ameagiza mkulima akatwe kutokana na uzito wa mfuko sio kukadiria kilo moja.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha wakulima kupitia mazao wanayozalisha kwa kuwaongezea elimu ya Kilimo bora na chenye tija.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo mkoani Simiyu kwa ajili ya sherehe za wakulima (Nanenane) ambazo kilele chake ni tarehe 8 Agosti 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga maadhimisho hayo akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post