WAZIRI JAFO ATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI 2019

Serikali imewachagua wanafunzi 1,674 kujiunga kidato cha tano baada ya awamu ya kwanza kukosa fursa hiyo.

Awali, serikali ilitangaza kuwa wasichana wote waliofaulu kidato cha nne walichaguliwa kujiunga vyuo mbalimbali pamoja na kidato cha sita lakini wavulana 1,861 hawakuchaguliwa licha ya kuwa na sifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza hayo leo, Jumatano (Agosti 28, 2019), jijini Dodoma huku akisema kuwa 187 wamekosa kwa kukosa uwiano katika tahasusi zao.

Waziri Jafo amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16,2019 huku akiwataka waliokosa nafasi kutokata tamaa badala yake waombe vyuo vya kati ili wajiunge.

Ametaja sababu za kupatikana kwa nafasi ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kujiunga shule binafsi na baadhi ya shule zimeongeza majengo.
Hii hapa orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano, 2019 Awamu ya Pili (Second Selection)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527