WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 23 KWA MAAFISA MAENDELEO KATA KWA JIJI LA DODOMA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Seleman Jafo ameshiriki kwa pamoja kikao cha Baraza la madiwani jijini Dodoma na kukabidhi pikipiki   23 kwajili ya maafisa maendeleo ya kata na kulipongeza jiji hilo kwa kazi kubwa linazofanya.

Waziri jafo ameyasema hayo Jijini hapa katika kikao cha Baraza la Madiwani pamoja na kukabidhi pikipiki  kwa maafisa hao, huku akiwataka madiwani hao kuwa na upendo ili kuweza kuipelekea Dodoma mbele.

Aidha, Waziri jafo amewataka kutokubezana,kunyong’onyeshana ,unyanyapaa kwani kuna baadhi ya watu katika maeneo mengine wamekuwa na tabia ya kunyanyapaa wenzao na kwa kufanya hivyo si sawa.

Katika hatua nyingine Waziri jafo amempongeza mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma  Godwini Kunambi ,kwa kazi kubwa anayoifanya , kwani katika wakurugenzi  wanaojitahidi, amekuwa akifanya vizuri katika uongozi wake.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bwana Godwin Kunambi amesema kuwa uchangiaji wa miradi ya maendeleo umeongezeka  kutoka shilingi Bilioni 13.590  kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi kufikia shilingi Bilioni 54.352 kwa mwaka wa fedha 2018/2019  sawa na ongezeko la asimia 74.9%.

Mbali na hilo kunambi amesema halmashauri inajukumu jingine la kustawisha makao makuu ya nchi,huku akisema katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilikisia kukusanya  na kupokea jumla ya shilingi Bilioni 159,Milioni 467,35 elfu 337.

Patrobas Katambi ni mkuu wa wilaya ya Dodoma ametumia kikao hicho kumpongeza waziri jafo ,kwa kazi kubwa ambayo anaifanya  pamoja na na kusema kuwa katika utawala bora wamekuwa wakisimamiana vizuri kuweza kuhakikisha kuwa sheria,kanuni ,taratibu,kanuni ,miongozo na maagizo ya viongozi yanafuatwa.

 Hatahvyo, Kunambi amesema bajeti ya Halmashauri iliongezeka kutoka  shilini Bilioni 20.798 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi shilingi Bilioni 67.149 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 69.02% ya makadirio ya mapato ya ndani.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527