WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI WATAKIWA KUIMARISHA LISHE


Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya lishe katika ngazi ya jamii ili kupunguza hali ya udumavu kwa jamii.


Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwenye kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini hapo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwe na taifa lisilo na kiwango cha chini cha hali ya lishe waganga wakuu hao lazima wapange mikakati ambayo itaanzia ngazi ya jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa lishe bora na inayostahili kwa familia hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili mikakati hiyo ifanikiwe.

Hata hivyo alisisitiza watoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuimarisha huduma za afya katika maeneo yao ili wananchi wanaoenda kupata huduma wapate huduma hizo kwa haki na usawa” na katika hili ni vyema mwananchi anayekuja kupata huduna ni vyema aridhike na huduma anayopata katika vituo vyetu vyote nchini”.Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwataka waganga wakuu hao kusimamia utendaji wa kazi katika maeneo yao ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii“inasikitisha kuona mama mjamzito anafariki kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uzembe au kutokupata huduma sahii jambo hili halikubariki”.

Kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri mwaka huu kinafanyika jijini hapa ambapo kilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na kauli mbiu ya kikao hicho ni “Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati na utakua wa siku tano.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post