WAANDAMANAJI WACHOMA JENGO LA BUNGE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 21, 2019

WAANDAMANAJI WACHOMA JENGO LA BUNGE

  Malunde       Wednesday, August 21, 2019

Maelfu ya Waandamanaji katika Jimbo la Indonesia  la Papua Magharibi jana wamechoma moto jengo la Bunge wakipinga kile wanachodai ni kukamatwa na kudhalilishwa kwa Wanafunzi.

Waandamanaji hao waliokuwa wakipinga vitendo hivyo vya udhalilishaji wanavyodai vinafanywa na vyombo vya dola dhidi ya Wanafunzi wa Papua, pia waliweka vizuizi barabarani.

Wanafunzi 43 katika maeneo ya Surabaya na Java Mashariki walikamatwa siku ya maadhimisho ya uhuru wa Indonesia baada ya bendera ya nchi hiyo kukutwa nje ya nyumba zao zikiwa zimeharibiwa.

Aidha, msemaji wa Polisi wa Java Mashariki, Frans Barung Mangera amesema kuwa wanafunzi hao waliachiwa huru baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa kutokana na kukosekana vithibitisho kuwa waliharibu bendera hizo.

Hata hivyo, waandamanaji walipatwa na hasira baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha Polisi wakiwa na Wanajeshi wakiwaita Wanafunzi hao ‘Nyani’ na ‘Mbwa’

Gavana Msaidizi wa eneo hilo, Mohammad Lakotani amesema kuwa wakati mazungumzo yakiwa yanaendelea kati ya waandamanaji na Mamlaka, maandamano hayo yameharibu uchumi wa Papua Magharibi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post