Video : WATANZANIA WAANDAMANA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI KUSHINIKIZA NDEGE YA AIR TANZANIA IACHIWE


Mmoja wa Waandamanaji akiwa amebeba bango lake nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania leo,wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa sasa. 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV
TUNATAKA ndege yetu...tunataka ndege yetu...Mandela anahujumiwa ...tunataka ndege yetu...! Hivyo ndivyo walivyokuwa wanaimba Watanzania walioamua kufanya maandamano katika Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa sasa.

Wananchi hao wameamua kwenda kwenye Ubalozi huo leo Agosti 28,mwaka huu wa 2019 kati ya saa nne na saa tano asubuhi huku wengine wakionekana kuwa na hasira kali wakiwa na mabango.

Wakiwa kwenye ubalozi huo Watanzania hao walikuwa wanapaza sauti ya kutaka ndege hiyo kuachiwa haraka na kinachofanywa na Afrika Kusini ni kuihujumu Tanzania pamoja na kumhujumu Mandela.

Wakati wakiwa katika ubalozi huo wananchi hao walikuwa wameshika mabango yanayoshinikiza ndege hiyo kuachiwa.

Baadhi ya wananchi wamehoji waliokuwepo kwenye ubalozi huo walikuwa wanahoji inakuaje suala la mtu binafsi linaigharimu Serikali ya Tanzania. Wengine wamesema inashangaza kuona marafiki wa Tanzania kwa miaka mingi ambao ni Afrika Kusini wakiahiriki kurudisha nyuma maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza akiwa eneo la tukio Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema sio sahihi kwa wananchi hao kwenda katika ubalozi huo,hivyo amesema watu watatu ambao ni vinara wa maandamano hayo wanawashikilia kwa sasa

"Hata kama walikuwa na haki ya kuandamana hapaswi kufanya hivyo kwasababu ni kinyume na sheria,waache suala hilo lishughulikiwe na Serikali kwa utaratibu unaofaa kwani tayari maofisa wa ngazi za juu wanaendelea kulishughulikia,"amesema Mambosasa.

Hata hivyo eneo hilo nilikuwa limeimarishwa na ulinzi qmbapo Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU)walikuwa eneo la ubalozi huo wakisimamia usalama.Polisi waliamua kuwatawanya wananchi waliokwenda katika ubalozi huo.

Watanzania hao ambao walionekana kuwa na hasira kutokana na ndege yao kushirikiwa nchini Afrika Kusini kwa siku kadhaa waliuzunguka waliamua mazingira Ubalozi huo huku waiomba vyombo za kutaka ndege inayoshikilliwa kuachiwa haraka.
 Baadhi ya Wananchi wakiwa wameandamana nje ya ubalozi Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania kabla ya kutawanywa na jeshi la Polisi,wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa saa.

Ndege hiyo ya ATCL aina ya Airbus A220-300, ilizuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwishoni mwa wiki iliyopita kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng nchini humo.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527