AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMNAJISI MTOTO ILI AJIRIDHISHE KINGONO

Raia wa Malawi, Paul John (30), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kunajisi mtoto wa miaka saba ili ajiridhishe kingono.


Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hellen alidai Machi 25, mwaka huu eneo la Tegeta Nyuki wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alimuingiza vidole sehemu za siri mtoto wa miaka 7.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka na Hakimu Mwakalinga alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili Watanzania,  wafanyakazi wa taasisi inayotambulika kisheria, barua kutoka kwa waajiri wao na vitambulisho vya kazi.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 10.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527