TIGO YAING'ARISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

Rosemary Mroso kutoka kitengo cha huduma kwa wateja Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania akimhudumia mteja wa kampuni hiyo Emmanuel Liwimbi Ofisa Huduma za Mikutano Mwandamizi kutoka Sekretarieti ya SADC alipotembelea banda hilo kwenye mkutano wa SADC unaoendelea katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Tigo ni mdhamini wa huduma za intaneti katika Mkutano huo.

Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC   jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu  wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.
Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akimsikiliza mteja wa kampuni hiyo Bw. Selemani Kifyoga aliyefika kwenye banda hilo kwa ajili ya kusajili laini yake ya simu kwa mfumo wa kutumia vidole. Tigo ni miongoni mwa wadhamini katika mkutano unaondelea wa SADC
Mfanyakazi wa  Tigo akitoa huduma kwa wateja waliofika katika banda lake lililopo ndani ya Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo Mkutano Mkuu wa 39 wa marais wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika. Tigo ni  mdhamini mkuu wa Huduma ya intaneti katika mkutano huo.  


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527