RAIS MAGUFULI AAHIDI USHIRIKIANO SADC, AIPIGIA CHAPUO LUGHA KISWAHILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Ndani cha Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akihutubia katika mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Wakuu mbalimbali wa nchi za SADC wakati wa wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kuaza kwa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 
Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Wake wa Marais pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam 
RAIS Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa kwa niaba ya watanzania anaahidi ushirikiano wa hali ya juu na nchi jumuiya wanachama ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwa kivitendo zaidi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi rasmi wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali Rais Magufuli amesema kuwa tangu jumuiya hiyo ianze mwaka 1980 malengo yalikuwa ni kupambana na ukoloni pamoja na kujenga ushirikiano katika kujenga uchumi miongoni mwetu.

"Ni miaka 20 tangu ufanyike mkutano huu akiwepo mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa niaba ya watanzania tunahaidi ushirikiano ili ndoto za Mwalimu Julius Nyerere na waanzilishi wa jumuiya hiyo yaendeele kufanyika kwa vitendo zaidi" ameeleza Magufuli.

Magufuli amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo lugha ya Kiswahili imekuwa ikitumiwa ndani ya jumuiya katika harakati za ukombozi wa kupambana na ukoloni na aina zote za ubaguzi pamoja na kuwaunganisha wanajumuiya, na kwa sasa lugha ya Kiswahii ni moja kati ya lugha 10 duniani ikizungumza katika nchi kumi duniani na ikizungumzwa katika nchi sita za ukanda wa SADC hivyo Kama wanajumuiya hatuna budi kuichagua lugha ya Kiswahii kuwa lugha Kiswahili kuwa rasmi ya nne ya jumuiya yetu ya SADC.

Awali akizungumza katika mkutano huo katibu mtendaji mkuu wa SADC Dkt. Stergomena Tax ameipongeza Tanzania kwa kuwa nchi pekee kukidhi vigezo katika ukuaji wa uchumi na kufikia asilimia 7 huku akipongeza utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati na miundombinu.

Aidha Dkt. Tax amezipongeza nchi jumuiya kwa kuwa kutunza amani na utulivu na kushauri kushirikiana na taasisi za sekta binafsi ambazo kwa kiasi kikubwa huchangia mapato kwa serikali, kutoa ajira pamoja na kuimarisha hali za uchumi kwa wananchi.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi, viongozi wa serikali, viongozi wastaafu na mabalozi ambapo ndani ya siku mbili watajadili masuala mbalimbali ya kiuchumi na Rais Magufuli atapokea kijiti cha uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa muhula mmoja kutoka kwa Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post