WAZIRI MKUU ATOA ONYO LA MWISHO KWA MKURUGENZI MANISPAA YA SHINYANGA KUGOMBANA NA WENZIE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi pamoja na Mwekahazina wa Manispaa hiyo, Pascal Makoye, ambapo amewataka wabadilike na waache kugombana na badala yake watekeleze majukumu yao.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo Agosti 9, 2019, wakati akizindua nyumba 10 za Askari Polisi katika Manispaa ya Shinyanga eneo la Kambarage, mradi ambao umetokana na fedha kiasi cha sh. milioni 225.

Waziri Mkuu amesema viongozi hao wameshindwa kutekeleza majukumu yao, ikiwemo kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji wa mapato, na kutoa kazi hiyo kwa kampuni zisizokuwa na uwezo.

“Mkurugenzi na wenzako nawaonya kwa mara ya mwisho badilikeni na hakikisheni mnatekeleza majukumu yenu ipasavyo yakiwemo ya ukusanyaji wa mapato.” amesema Waziri Mkuu.

Kuhusu nyumba za Askari Polisi, Waziri Mkuu amesema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuhakikisha askari wanaishi katika mazingira mazuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527