MWANAMKE ALIYETEMBEA NA WANAUME 221 ACHOKA KUVALISHWA PETE BILA KUOLEWA....AFUNGA NDOA NA MBWA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 5, 2019

MWANAMKE ALIYETEMBEA NA WANAUME 221 ACHOKA KUVALISHWA PETE BILA KUOLEWA....AFUNGA NDOA NA MBWA

  Malunde       Monday, August 5, 2019

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Elizabeth Hoad raia wa Uingereza,  amefunga ndoa na Mbwa wake aitwaye Logan katika kipindi cha Television Nchini humo.

Baada ya kufunga ndoa, Mwanamke huyo ameeleza aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Wanaume 221, kati ya hao Wanne ndio walimvalisha pete ya uchumba lakini imeshindikana kuolewa.

Pia mwanamke huyo amesema ameamua kufunga ndoa na Mbwa wake "Logan", kwa sababu ya kuchoshwa na Tabia za Wanaume wazee kupenda Wanawake wadogo na Wanawake wadogo kupenda Wanaume wazee.

Aidha Elizabeth ameendelea kusema Mbwa huyo ana maana kubwa sana kwake kwa sababu wameshasaidiana kwa vitu vingi hasa wakati alipoumizwa na Wanaume ambao aliwahi kuwa nao, pia ana marafiki zake 10 ambao wameamua kufunga ndoa na Mbwa wao.

Akiweka kiapo katika sherehe ya kufunga ndoa hiyo Elizabeth aliahidi kuwa, "kwa mwili wake wote atatembea na Mbwa Logan, atamjali na kumpenda siku zote za maisha yake na kulala nae kitanda kimoja" amesema Elizabeth.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post