MWANAHARAKATI STELLA NYANZI AHUKUMIWA KIFUYNGO CHA MIEZI 18 KWA KUMTUSI RAIS MUSEVENI WA UGANDA


Mwanaharakati msomi wa Uganda Dkt. Stella Nyanzi amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.

Nyanzi amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kimtandao dhidi ya Rais Yoweri Museveni na familia yake.

Dr. Nyanzi alikataa kumsikiliza hakimu akisoma hukumu dhidi yake na badala yake kufanya vurugu kwa kuvua nguo na kuonesha sehemu ya mwili wake.

Mwanaharakati huyo hakuwa mahakamani lakini hukumu dhidi yake ilitolewa kupitia video link kutoka jela.

Wakati kesi ikiendelea Bi. Stela alikataa kuomba dhamana na amekuwa katika gereza kuu la Uganda la Luzira kwa miezi minane. Sasa atazuiliwa gerezani kwa miezi tisa zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527