MO DEWIJ AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI WA SIMBA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 31, 2019

MO DEWIJ AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI WA SIMBA

  Malunde       Saturday, August 31, 2019

Mwekezaji wa simba SC  Mohamed Dewij amefunguka na kuonyesha jinsi alivyoumizwa na matokeo mabaya ya timu ya Simba dhidi ya wapinzani wao kutoka Msumbiji UD Songo katika michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kutolewa mapema kwenye michuano hiyo

Hii imekuja baada ya Simba kupata sare ya 1-1 wakati mchezo wa kwanza nchini msumbiji matokeo yalikuwa 0-0, hivyo goli la ugenini liliwabeba UD Songo na Simba kutupwa nje ya michuano licha ya msimu uliopita kufanya vizuri kwa kufika hatua ya robo fainali.

Kupitia kiurasa zake za mitandao ya kijamii Mo Dewij ameandika hivi:-

Wanasimba, mnisamehe kwa ukimya. Maumivu ya matokeo yametupata sote. Naomba tukumbushane: Sisi ni SIMBA! Simba lazima anyanyuke! Hawezi kukata tamaa.

Niwaombe tusivunjike moyo wala kukata tamaa. Hatutaogopa maneno ya watu na hatutaacha kupambana na kujipanga kwa ajili ya malengo yetu. Msimu huu tutautumia kikamilifu kuhakikisha tunaboresha mipango yetu ili msimu ujao turudishe furaha kwa Wanasimba wote.

Tumwombe Mwenyezi Mungu atutangulie katika safari yetu endelevu. Tukumbushane tena: Roma haikujengwa kwa siku moja. Tuwe wavumilivu, tutafika tu Insha’Allah. 🙏🏽
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post