MATUMAINI YA KUPATIKANA DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA EBOLA YAANZA KUONEKANA


Wizara ya Afya katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imesema dawa mbili za majaribio ya kuutibu ugonjwa wa Ebola zinaonekana kuyanusuru maisha ya wagonjwa.
 

Dawa hizo zinazotokana na kingamwili ,za watu walionusurika na ugonjwa huo hatari zimeonyesha mafanikio mema miongoni mwa wagonjwa waliozitumia, katika juhudi za kupambana na mripuko wa sasa wa Ebola Mashariki mwa Kongo. 

Aina nne za dawa zilikuwa zikifanyiwa majaribio, lakini aina mbili, REGN-EB3 na mAb114 zilionekana kuleta tija. Mbili nyengine, ZMapp na Remdesivir sasa imeamuliwa zisitumiwe. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimarekani kwa ajili ya magonjwa ya kuambukiza Antony Fauci amesema mafanikio ya dawa hizo ni habari njema, ambazo zinaashiria kupatikana tiba dhidi ya maradhi ambayo katika kipindi cha hivi karibuni hakuna aliyekuwa akifikiria. 

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limewahimiza wagonjwa wa Ebola kutafuta dawa hizo haraka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post