UMOJA WA MATAIFA UNACHUNGUZA VISA 35 VYA MASHAMBULIZI YA KIMTANDAO YA KOREA KASKAZINI


Wataalam wa Umoja wa mataifa wanasema wanachunguza visa visivyopungua 35 kutoka nchi 17 ambazo raia wa Korea Kaskazini wanatumia mashambulizi ya mtandao kupata fedha kinyume cha sheria ili kufadhili mpango wake wa nyuklia na kutoa wito wa kuwekewa vikwazo kwa meli zinazoipatia mafuta nchi hiyo.

Wiki iliyopita shirika la habari la Associated Press liliripoti likinukuu ripoti iliyotolewa na wataalam hao wa Umoja wa Mataifa kuwa Korea Kaskazini imekuwa ikijipatia hadi dala bilioni mbili kutoka kwenye shughuli zake za kufanya mashambilizi ya mtandao dhidi ya taasisi za kifedha na maduka ya kubadilishia fedha.

Ripoti hiyo imefichua kuwa taifa jirani la Korea Kusini ndiyo limeathiriwa zaidi na shughuli hizo za uvamizi wa kimtandao ikirikodi visa 10, ikifuatiwa na India iliyoshambuliwa mara 3 huku Bangladesh na Chile zilirekodi kila moja visa viwili. 

Mataifa mengine 13 yamerikodi kisa kimoja kimoja cha mashmbulizi ya mtandao kutoka Korea Kaskazini.

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527