DEREVA LORI LA MAFUTA LILILOTEKETEA KWA MOTO RUVUMA APATIKANA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 13, 2019

DEREVA LORI LA MAFUTA LILILOTEKETEA KWA MOTO RUVUMA APATIKANA

  Malunde       Tuesday, August 13, 2019

Dereva Hurbet Mpete aliekuwa anaendesha lori la mafuta lililopata ajali Mkoani Ruvuma amepatikana akiwa hai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa  amesema dereva huyo ana michubuko kidogo na amevunjika mbavu, hivyo wamempeleka Hospitali kwa matibabu zaidi.


RPC Marwa amesema uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo ingawa  shehena ya mafuta lita 33,000 alizobeba zimekutwa salama na mmiliki wa mafuta hayo ameshahamisha.Lori hilo mali ya James Mwinuka ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Njombe Filling station  lilipata ajali juzi Jumapili Agosti 11,2019 saa 4 usiku  baada ya kuacha  njia na kugonga mti Kijiji cha Hangangadinda mkoani Ruvuma. Katika ajali hiyo, kichwa chote cha Lori hilo kiliteketea kwa moto na kubakiza tank pekee lililokuwa na Lita 33, 000 za Petrol.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post