Kampuni ya Huawei imeweka wazi jina la programu endeshaji mpya kwa ajili ya simu na vifaa vya kisasa vya kielektroniki ambayo itaanza kutumika badala ya Android.
Mfumo huo wa Huawei-HarmonyOS unalenga kupunguza utegemezi wake kwa kampuni za Marekani.
HarmonyOS utakuwa tayari kuwekwa katika skrini za samart kwenye bidhaa kama vile Televisheni, saa za smart , na magari baadae mwaka huu, amesema Richard Yu, Mkurugenzi mkuu wa wa kitengo cha walaji cha Huawei katika mkutano wa ubunifu.
Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Huawei,kampuni ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani ya mauzo ya smartphone , imesema itaangalia jinsi ya kuuweka mfumo wa HarmonyOS kwenye vifaa zaidi zikiwemo simu zake za mkononi aina ya smartphones.
Kampuni ya Huawei inasema kuwa imeazimia kuendelea kutumia Android ,lakini HarmonyOS utatumika kama mpango mbadala kama mambo yataenda kombo
Tangazo hilo la Huawei limekuja miezi kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuweka masharti ya kibiashara nchini Marekani yanayoilenga kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine washirika .
Serikali ya Marekani imeishutumu Huawei kwa kuiba siri za kibiashara , na ikasema inaleta hatari kwa usalama wa taifa.
Baada ya shutuma hizo , Google, Intel,na makumpuni mengine yanayochangia kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na utatuzi wa matatizo ya smartphone walisitisha biashara na Huawei
Social Plugin