Picha : WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA




Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, wamepewa mafunzo namna ya kuandika habari zenye tija ndani ya jamii, ambazo zitatatua matatizo yao na kuleta furaha kwa wananchi.


Mafunzo hayo yametolewa leo Agosti 23,2019 na Mwezeshaji Dastani Kamanzi kwenye mafunzo ya waandishi wa habari, ambayo yanaendelea Jijini Mwanza kwenye ukumbi wa mikutano Belmont Hotel, yanayoendeshwa na mtandao wa asasi ya kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), Chini ya kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC).


Mafunzo hayo yana husisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Kagera pamoja na Kigoma, yenye mlengo wa kuongeza tija kwa waandishi hao, katika kuandika habari zenye kutoa elimu ya uraia kwa umma pamoja na uchaguzi.


Kamanzi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era la Jijini Dar es salaam, amesema Mwandishi mwenye tija ni yule ambaye ana andika habari zenye mguso ndani ya jamii na kuweza kuwatatulia matatizo yao pamoja na kuleta, uhuru, haki, amani pamoja na udungu.


“Mwandishi wa habari mwenye tija ni yule ambaye ana andika habari zenye mguso ndani ya jamii pamoja na kutatua matatizo yao, na kuleta furaha kwa umma pamoja na Serikali,”amesema Kamanzi.


“Ili uwe Mwandishi wa habari mwenye tija lazima uzingatie maadili ya taaluma yako, mjuzi katika teknolojia inayotawala taaluma yako, Mwadilifu, pamoja na kujua habari unayotaka kuandika inafaida gani ndani ya jamii, na siyo kujiandikia tu habari bila ya kujua matokeo yake,”ameongeza.


Naye Mwezeshaji Ndimara Tegambwage ambaye ni Mwandishi Mwandamizi hapa nchini, amewataka waandishi wa habari za uchaguz wazingatie Shajala ya Ripota (dairy), ili wawe na kumbukumbu za uchaguzi, na kuweza kuandika habari nzuri, kipindi kabla ya uchaguzi, kipindi cha kupiga kura, na kipindi baada ya uchaguzi.

Anasema Mwandishi wa habari anapokuwa na Shajala hiyo ya Ripota, itamsaidia kujua historia ya uchaguzi kwenye eneo husika ama jimbo, na kuweza kuandika habari za uchambuzi, kisiasa, kiuchumi, kiusalama. Chakula, miundombinu, pamoja na kuweza kuwabana wagombea juu ya ahadi walizoahidi kabla ya uchaguzi.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Dastani Kamanzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari zenye Tija kwa jamii na kutatua matatizo yao. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog 

Mwandishi wa habari mwandamizi Ndimara Tegambwage ambaye pia ni mhariri wa gazeti la Mwananchi akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari,kipindi kabla ya kupiga kura, kipindi cha kupiga kura, na kipindi baada ya kupiga kura.

Mwandishi wa habari mwandamizi Ndimara Tegambwage ambaye pia ni mhariri wa gazeti la Mwananchi, akitoa mafunzo wa waandishi wa habari kuwa na Shajala Ripota ambayo itamsaidia kuandika habari vizuri za uchaguzi.

Mwezeshaji Jimy Luhende akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari za uchaguzi katika nyanja mbalimbali.

Mwandishi wa mitandaoni Nicholaus kirunga kutoka Kigoma akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Aidani Mhando wa Chanel Ten kutoka Mkoani Simiyu akichangia mada kwenye mafunzo ya wana habari Jijini Mwanza.

Mwandishi wa habari Rhoda Ezekiel kutoka Gazeti la Uhuru mkoani Kigoma akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza yanayohusu uandishi wa habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Joel Maduka kutoka Storm FM Mkoani Geita, akichangia mada kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Kigoma, Kagera, Mara, na Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi na zenye Tija kwa umma.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Mafunzo yanaendelea.

Mafunzo yanaendelea.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo Jijini Mwanza.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527