POLISI MBEYA WAZUNGUMZIA TUKIO LA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA KUVAMIWA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 29, 2019

POLISI MBEYA WAZUNGUMZIA TUKIO LA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA KUVAMIWA

  Malunde       Thursday, August 29, 2019

Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudi Kitta
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Jeromi Ngowi, amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wale wote waliohusika na kuvamia msafara wa Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudi Kitta, katika Kijiji cha Mpunguti wilayani humo.

Kamanda Ngowi amesema kuwa msafara huo haukutekwa bali ulishambuliwa kwa mawe na kwamba Mkuu wa Wilaya na wenzake wako salama na hali ya usalama na utulivu imekwisharejea.

''DC na wenzake wako salama hali ya  amani na utulivu imerejea mimi nipo eneo la tukio, kuna bwana amefariki kwenye uwanja wa mpira wananchi wakawa wanahisi mama yake mzazi amemuua kwa imani za kishirikina, maiti ilipotaka kuzikwa wakakataa wakamtaka mama yake amfufue" amesema Kamanda Ngowi.

Aidha Kamanda Ngowi ameongeza kuwa, "Hakuna mtu ambaye amelazwa wala kujeruhiwa, isipokuwa vurugu zilikuwa kubwa kidogo ila walijitahidi kutumia mbinu kujiokoa na sisi tuliwahi kufika na kuwasaidia, bado nipo hapa ili kufuatilia zaidi kujua waliohusika na vurugu hizo.".

Inaelezwa kuwa vurugu hizo zilianza juzi siku ya Agosti 27, 2019.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post