CHAVITA TANGA WATAKA WAKALIMANI KILA KITUO WAKATI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAACHAMA cha Viziwi mkoani Tanga (Chavita) wametoa wito kwa serikali kuweka wakalimani katika kila kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kurahisisha mawasiliano kwao.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Chama hicho mkoani Tanga Nassoro Ally wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake ambapo alisema pia wanatoa wito kwa serikali kuwaboreshea mazingira kwa kuwapatia elimu ya uraia

Alisema kwani uwepo wao kwenye maeneo husika itawasaidia na kuwawezesha kuweza kutekeleza wajibu wao kwa waledi mkubwa kwa kutimiza haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi ambao wanaweza kuleta maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka kwenye chaguzi hizo.

“Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nitoa wito kwa serikali kuona namna bora ya kuweza kuweka wakalimani kwenye vituo vyote vya kupigia kura kwa lengo la kurahisisha mawasiliano “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo zinawakabili alisema kwamba kubwa inayowakabili ni kukosekana kwa ushirikishwaji katika vyombo vya kutoa maamuzi ngazi ya mkoa na wilaya.

Aidha alisema pia vikwazo nyengine wanavyokutana navyo ni kuwepo kwa urasimu katika utoaji wa huduma za kijamii unaofanywa na maafisa ustawi wa jamii pindi wanapofuatilia hazi zao kwa kupewa majibu ya kuwakatisha tamaa.

Katibu huyo alisema pia vikwazo vingine kwao ni kutokuwa na uwazi katika utoaji wa huduma kwa makundi maalumu jambo ambalo limekuwa likiwakwamisha kwenye baadhi ya mambo muhimu kwao. 

“Katika hili tunatoa ushauri kwa serikali iwe inafuatilia kwa undani watoaji wa huduma kwani baadhi yao wanafanya kwa mazoea jambo ambalo linawapa wakati mgumu “Alisema

Hata hivyo alisema licha ya serikali kutenga asilimia 2 ya mapato ya ndani kwa ajili ya huduma kwao lakini wananyimwa fungu hilo kwa mwaka na asilimia 4 kwa ajili ya kukopesha walemavu upatikaji wake sio wa haki kwa sababu wanaunganishwa wasio na ulemavu.

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post